Kondomu za Dume ni chaguo la kwanza nchini Tanzania. Kondomu za Dume zinasambazwa nchini na shirika la T-MARC Tanzania kwa msaada wa shirika la maendeleo la Kimarekani (USAID). Ikiwa katika soko kwa miaka 9 sasa, Dume inalenga kuzuia maambukizi ya VVU miongoni mwa jamii iliyo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi. Kondomu ya Dume ina nembo ya triple tested, yaani imepitia vigezo vitatu vya viwango vya kitaifa na kimataifa (ikiwemo WHO, ISO na TBS) kwa hiyo kondomu ya Dume ina uwezo mkubwa wa kukukinga na kukulinda.